Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi angecheza Hispania, Italia

Lionel Messi Xxxxxx Messi angecheza Hispania, Italia

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika michuano ya Euro inayoendelea kwa sasa nchini Ujerumani, Lionel Messi angeweza kuwa anaichezea moja kati ya timu, kama sio Hispania basi Italia.

Mshindi huyu wa tuzo ya Ballon d’Or mara nane ambaye kwa sasa yupo Marekani akiitumikia Argentina katika michuano ya Copa America angeweza kuichezea Hispania mahali ambako aliwasili akiwa na umri wa miaka 13.

Messi mwenye umri wa miaka 37, baada ya kusaini na Barcelona aliishi Hispania kwa miaka mitano kabla ya kuanza kucheza katika timu za vijana za Argentina.

Katika kipindi hicho Chama cha soka cha Hispania kilijaribu kutaka kuwashawishi wazazi wake achezee taifa hilo lakini ilishindikana.

Messi alikuwa akiruhusiwa kuichezea Hispania kwa sababu babu yake ambaue alizaliwa Catalona, pia ana ndugu ambao walikuwa wakiishi hapo wakati yeye anatua Barcelona.

Mazungumzo yalichukua muda mrefu baina ya Chama cha Soka cha Argentina lakini mwisho Messi akaichezea Argentina.

Pia staa huyu alikuwa anaweza kuichezea Italia kwa sababu baba yake babu yake aliwahi kuishi huko miaka mingi iliyopita, hivyo alikuwa anaweza kupata uraia wa Italia.

Historia inaonyesha kwamba mzee huyo aliondoka Italia na kwenda zake Argentina katika Mji wa Rosario mwaka 1883.

Hata hivyo, hakukuwahi kuwa na mazungimzo baina ya Chama cha soka cha Italia na familia ya Messi ili kumshawishi achezee nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live