Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi anaendeleza balaa huyo

Lionel Messi Argentina V Australia World Cup 2022 3 Messi anaendeleza balaa huyo

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lionel Messi amefunga mabao mawili kwa timu ya Taifa ya Argentina

Messi ametokea kuwa mfungaji bora wa wakati wote kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mataifa ya Amerika Kusini, akifunga mabao yote mawili dhidi ya Peru.

Messi (36) alicheka na nyavu dakika ya 32 na kuongeza bao jingine baadaye kidogo. Kwa sasa amefikisha mabao 31, akimzidi Luis Suarez, 29 wa Uruguay.

“Hii timu ni matata, kila mara wakicheza wanaonekana kuwa wazuri zaidi katika historia,” Messi akasema baada ya mechi hiyo, akiongeza kwamba kwa maana ya kiwango cha gemu, wamejiongeza na kujiamini sana, wakiwa pia imara kila idara.

Mshambuliaji huyo alikosa fainali na klabu yake ya Inter Miami kwenye US Open Cup walikofungwa na Houston Dynamo mwezi uliopita, kutokana na majeraha na hakuwa ameanza mechi yoyote tangu Septemba 21. Aliingia akitokea benchi kwenye ushindi wa Argentina wa 1-0 dhidi ya Paraguay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live