Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi amwita mchambuzi 'punda'

Jamie Carragher Messssi Messi amwita mchambuzi 'punda'

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa soka na mchambuzi, Jamie Carragher amedai alipokea ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Lionel Messi ambapo supastaa huyo wa Argentina alimwita ‘punda’ kwa Lugha ya Kilatini.

Hiyo ni baada ya Carragher kumkosoa Messi wakati PSG ilipokuwa ikicheza Ligi Mabingwa Ulaya wiki iliyopita. Messi aliibuka na kutuma ujumbe huo ambao ulimshtua Carragher.

Alipoulizwa kama alipokea ujumbe kutoka kwa nyota huyo anayekipiga Inter Miami kupitia Kituo cha televisheni cha CBS Sports alijibu ndio.

“Aliandika kwa Lugha ya Kispanish, Argentina kwani wanazungumza Kispanish? Messi aliandika ‘Burro’ sikujua alimaanisha nini?” Baadaye mtangazaji wa kituo hicho akamuelewesha Carragher maana ya neno hilo kwamba ni punda.

Kwa mujibu wa ripoti maoni ya Carragher yalimuathiri staa huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye aliondoka PSG baada ya kudumu kwa muda wa miaka miwili.

Katika mchezo huo, PSG ilishinda mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dortmund kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Kylian Mbappe na Achraf Hakimi.

Carragher alikuwa akimponda Messi kwamba alikuwa akizingua wakati alipokuwa akiitumikia timu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live