Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi ampiku Ronaldo, aweka rekodi hii UEFA ...

Lionel Messi Lapulga.jpeg Messi ampiku Ronaldo

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nyota wa Paris-Saint Germain, Lionel messi amempiku Cristiano Ronaldo baada ya kufunga timu 39 katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya.

Miamba hiyo kutoka Ufaransa ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Maccabi Haifa dakika ya 24 tu ya mtanange huo lililowekwa kimiani na Tjaronn Chery kabla ya Messi kusawazisha.

Ronaldo alizifunga timu 38 tofauti katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya, awali alikuwa sawa na mpinzani wake lakini sasa amempiku.

Licha ya Ronaldo kutoshiriki Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu ameendelea kushikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo wa muda wote, kwani mkali huyo amefunga jumla ya mabao 140 huku Messi akicheka na nyavu mara 126.

Ronaldo ameshindwa kunga’ra michuano ya Europa wiki iliyopita mashetani wekundu wakipokea kichapo cha bao 1-0 ilipomenyana na Real Sociedad hatua ya makundi.

Messi amebeba jumla ya makombe manne ya Ligi Mabingwa Ulaya smimu wa 2006, 2009, 2011 na 2015 wakati Ronaldo akibeba matano kuanzia msimu wa 2008 2014, 2016, 2017 na 2018.

Mabao mengine ya PSG yaliwekwa kimiani na Kylian Mbappe na Neymar Jr, ushindi huo unakuwa wa pili mfululizo hatua ya makundi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz