Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi alibeba soka la Marekani

Lionel Messi Vs Parag Lionel Messi

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Gwiji wa soka wa Marekani, Clint Dempsey anaamini kuwasili kwa Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami kumekuza soka Marekani.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha ESPN, Dempsey alisema; “Ninaweza kuelezea Messi alipokuja mashabiki wa soka na Marekani kwa jumla wamezingatia na wameanza kufuatilia soka. Messi alipokuja Marekani alibadilisha kila kitu, alikuja utafikiri tumebeba Kombe la Dunia.”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amefurahia kuvaa jezi ya pinki tangu ajiunge na Inter Miami Julai mwaka huu

Tangu alipotua amefunga mabao 11 katika mechi 13 katika michuano yote na kutoa asisti tano. Pia aliisaidia klabu yake kushinda Kombe la kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Nahodha huyo wa Argentina aterejea dimbani kuiwakilisha Argentina dhidi ya Peru katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 Oktoba 17.

Wakati huo huo, Lionel Messi anashika namba mbili katika orodha ya wachezaji wanaolipwa pesa ndefu kwa mujibu wa jarida maarufu Forbes akiwa ameachwa mbali sana na mpinzani wake, Cristiano Ronaldo ambaye anashika nafasi ya kwanza kwani analipwa Pauni 214 milioni huku yeye akiwa analipwa Pauni 111 milioni.

Staa mwenzake wa zamani wa Barcelona, Neymar yupo nyuma yake, akilipwa Pauni 92 milioni, akimpiku staa wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe. Mkali wa Ligi Kuu England, Erling Haaland anashika namba sita akikadiriwa kulipwa Pauni 48 milioni, wakati Mohamed Salah anafuatia akiwa analipwa Pauni 44 milioni kwa malipo ya ndani na nje ya uwanja.

Chanzo: Mwanaspoti