Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi akerwa na kanuni mpya ya soka

Messi 500 Goals Lionel Messi

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Inter Miami, Lionel Messi alionesha hasira yake juu ya sheria mpya ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani ‘MLS’ inayomlazimu mchezaji aliyejeruhiwa kukaa nje ya uwanja kwa dakika mbili.

Messi amesema, "Kanuni za aina hii ni mbaya," baada ya kutoka nje ya uwanja wakati wa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mwenyeji Montreal juzi Jumamosi (Mei 11).

Katika dakika ya 40 ya mechi, mlinzi wa Montreal, George Campbell, alimfanyia madhambi Mshambuliaji huyo wa Argentina.

Madaktari wa Miami walikimbilia eneo la tukio kumhudumia mchezaji huyo, lakini Campbell hakuoneshwa kadi ya njano kwa tukio hilo.

Kwa sababu ya kanuni mpya za mwamuzi hatasimamisha mpira kwa sababu ya jeraha la mchezaji ambaye atabaki uwanjani kwa zaidi ya sekunde 15 na madaktari kuingia uwanjani, mchezaji huyo anaweza kutakiwa kuondoka uwanjani kwa kwa dakika mbili."

Messi alitoka nje ya uwanja katika wakati muhimu, baada ya faulo hiyo kuamsha mpira wa adhabu kwa Miami katika nafasi nzuri kwa mchezaji huyo kufunga.

Katika kipindi kifupi cha kukaa pembeni, mchezaji huyo aligeukia kamera kuonesha dharau huku akitikisa kichwa kwa hasira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live