Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi ajiweka 'level' za Maradona Argentina, kabakisha hili tu!

Messi Lionel Lapulga Lionel Messi

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amefikia rekodi ya gwiji wa zamani wa taifa hilo Diego Maradonna kwenye michuano ya kombe la dunia. Hiyo ni baada ya kufunga katika mchezo wa juzi dhidi ya timu ya taifa ya Mexico.

Timu ya taifa ya Argentina juzi ilipata ushindi wake kwanza kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mexico, ambapo Messi aliweza kufikia rekodi ya gwiji Maradonna ya mabao nane kwenye kombe la dunia.

Nahodha huyo wa Argentina aliifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo huo ambapo lilikua bao lake la nane kwenye michuano hiyo tangu ameanza kucheza michuano hiyo mwaka 2006 akiwa bado kijana mdogo kabisa.

Baada kufunga katika mchezo huo Messi pia ameweza kumfikia hasimu wake wa muda wote Cristiano Ronaldo ambaye na yeye ana magoli nane katika michuano ya kombe la dunia tangu ameanza kucheza michuano hiyo mwaka 2006.

Nahodha huyo wa Argentina mpaka sasa amefanikiwa kua mfungaji bora wa muda wote kwenye taifa hilo na kumfikia gwiji Maradonna, Hivo jambo kubwa ambalo amelibakiza fundi huyo wa kabumbu ni kupelekea taji la kombe la dunia nchini Argentina kama Maradonna alivyofanya mwaka 1986 michuano iliyofanyika nchini Mexico.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live