Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi aipa Ubingwa Inter Miami, aandika rekodi mpya Duniani

Lionel Messi 1692504890 114379 Lionel Messi

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lionel Messi ameshinda kombe lake la 44 na kuwa mwanasoka mwenye makombe mengi zaidi katika historia ya soka baada ya kuiongoza klabu ya Inter Miami kushinda fainali ya kombe la ligi (League Cup) iliyomalizika asubuhi ya Agosti 20, 2023.

Inter Miami walishinda mchezo huo wa Fainali kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 10-9 baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Messi ameshinda tuzo mbili katika michuano hiyo akitwaa tuzo ya mfungaji bora baada ya kumaliza akiwa na magoli 10 pamoja na kuwa mchezaji bora wa mashindano.

Mlinda mlango wa Inter Miami, Drake Callender ndiye shujaa wa mechi ya fainali baada ya kufunga penalti ya mwisho huku akiokoa penalti ya golikipa wa wapinzani wao Nashville SC, Elliot Panicco.

Inter Miami imeshinda kikombe chake kwanza cha michuano ya Super Cup iliyoshirikisha timu 47 kutoka Ligi Kuu ya MLS ( Major League Soccer) ya Marekani na Ligi Kuu ya LigaMX ya Mexico.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live