Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi aiongoza Argentina kufuzu Kombe la Dunia 2022

Leo Messi Nahodha wa Argentina, Lionel Messi

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Paris Saint-Germain na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi ameongoza taifa lake kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 baada ya kupata sare dhidi ya Brazil.

Katika kundi hilo la nchi za Amerika kusini, Brazil na Argentina ni wazi wamefuzu kucheza michuano hiyo, wakati timu nyingine tatu zitachuana katika hatua ya mtoano.

Brazil ilikuwa timu ya kwanza kutoka Bara la America kufuzu katika michuano hiyo, wakati Messi akiiongoza Argentina hapo jana kupata sare ya tasa na kufwata nyayo hizo.

Kombe la dunia linatarajiwa kuwa na angalau timu 48 zitakazo shiriki mashindano ya 2022. Mchanganuo ufuatao utatumika kupata timu hizo kulingana na mabara husika.

AFC, Asia – Timu 4 au 5, CAF, Africa – Timu 5, CONCACAF, North, Central America na Caribbean – Timu 3 au 4.

CONEMBOL, South America – Timu 4 au 5, UEFA, Europe – Timu 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live