Lionel Messi kwa mara ya kwanza ameanza kuandika historia kwenye ligi kuu ya Ufaransa baada ya kufunga goli lake la kwanza kwenye ligi hiyo, huku wakibuka na ushindi wa 3-1 licha ya kuwa pungufu baada ya Keylor Navas kupewa kadi nyekundu.
Mbappe alikuwa wa kwanza kuiandikia PSG goli kabla Randal Kolo kurudisha huku Dennis Appiah akijifunga na Messi kuzima kabisa ndoto za Nantes kwa kufunga goli la tatu.
"Nina furaha ya kufunga goli langu la kwanza, nilihitaji sana hili" amesema messi baada ya mcchezo
Messi ameifungia timu ya PSG magoli 3 ila magoli yote amefunga kwenye michezo ya ligi ya mabingwa Ulaya, lakini alikuwa bado hajafanikiwa kuweza kupata goli kwenye ligi ya Ufaransa licha ya kucheza michezo mitano.
Lionel messi alikosa michezo miwili kabla ya kupisha mapumziko ya michezo ya kimatifa sababu ya majeruhi, lakini sasa amerudi akiwa na hamasa kubwa sana, PSG kwa sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 12 kutoka kwa anayemfuatia Rennes.