Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi aamua kuondoka PSG

Messi Aadhibiwa, Atupwa Nje Ya Kikosi Messi kuondoka PSG

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lionel Messi ameripotiwa kuwa ataondoka Paris Saint German mwisho wa msimu huu baada ya uhusiano wake na miamba hiyo ya Ufaransa kufikia hatua mbaya zaidi.

Messi amesimamishwa kwa wiki mbili kucheza, kufanya mazoezi na kupokea mshahara kwa kipindi hicho kutokana na safari yake ya Saudi Arabia ambayo haijaidhinisha na klabu hiyo.

Mkataba wa Messi klabuni hapo unatamatika mwisho wa msimu huku kukiwa hakuna dalili ya nyongeza ya mkataba mpya kutokana na uamuzi huo wa PSG.

Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa michezo duniani raia wa Italia, Fabrizio Romano amesema kuwa ana uhakika Messi anaondoka PSG kutokana na taarifa rasmi alizonazo yeye kutoka kwenye vyanzo vyake vya karibu na Messi.

"Lionel Messi ataondoka Paris Saint-Germain mwisho wa msimu huu. Hakuna shaka kuhusu hilo.

"Nyuma ya pazia ninazo taarifa kuwa kuna mazungumzo baina ya Messi na PSG na tayari (baba wa Messi) ameshawaandikia PSG kuhusu uamuzi wao huo tangu mwezi uliopita," amesema Fabrizio Romano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: