Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi: Tutafanya kweli Ligi Kuu Bara

Messi X Prisons Messi: Tutafanya kweli Ligi Kuu Bara

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Tanzania Prisons ikifungua pazia ya Ligi Kuu dhidi ya Singida Fountain Gate, straika wa timu hiyo Messi Roland amesema timu hiyo itafanya vizuri kutokana na maandalizi ya mapema waliyofanya huku akieleza mikakati yake.

Ligi Kuu inaanza kesho Jumanne kwa mechi tatu kupigwa viwanja tofauti na Ihefu itakuwa nyumbani dhidi ya Geita Gold, Namungo dhidi ya JKT Tanzania na Dodoma Jiji na Coastal Union.

Kwa upande wa Tanzania Prisons wao watashuka uwanjani Agosti 22 wakianzia ugenini mechi tatu mfululizo dhidi ya Singida FG, Azam FC na Tabora United kisha kurejea nyumbani dhidi ya Simba.

Nyota huyo raia wa Cameroon anatarajia kucheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza hapa nchini baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo ya jijini hapa.

Roland alisema kutokana na maandalizi waliyofanya kwa muda mwingi, wachezaji wamekuwa na muunganiko mzuri na makosa yaliyopo benchi la ufundi litayafanyia kazi kabla ya mechi hiyo.

Aliongeza, licha ya kuwa msimu wake wa kwanza kucheza soka la kulipwa hapa nchini, lakini haoni utofauti wowote kwani kama ni uwezo na uzoefu yuko fiti na hata hali ya hewa si mbaya.

“Tumekuwa na muda mzuri wa maandalizi na tutafanya vizuri, haijalishi tunaanzia ugenini, wachezaji tumekuwa na muunganiko mzuri na matarajio yetu ni kuanza kwa kishindo.”

“Binafsi nimejipanga licha ya kuwa ni msimu wa kwanza kucheza soka hapa Tanzania, ushirikiano na kujituma kwa kila mmoja ndio itakuwa chachu ya mafanikio,” alisema Roland.

Meneja wa timu hiyo, Laurian Mpalile alisema kiwango wanachoonesha nyota wao kwenye mazoezi kinawapa matumaini, nguvu na hamasa kuelekea kuanza msimu ujao.

Chanzo: Mwanaspoti