Lionel Messi amesisitiza hakutaka kuondoka Barcelona na akajiunga na Paris St-Germain kufuatia tofauti iliyotokea kati yake na klabu hivyo kutimkia Ufaransa na sasa anafurahia maisha akiwa na Inter Miami.
Mkali huyo mara saba wa tuzo ya Ballon d’Or alijiunga na Inter Miami sehemu ambayo amepiga hatua kwani katika mechi sita amefunga mabao tisa.
Na katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari akiwa mchezaji wa Inter Miami, Messi alifichua siri alitamani kuendelea kuichezea Barcelona, lakini alilazimishwa kuondoka katika klabu yake ya utotoni 2021 kutokana na matatizo ya uchumi.
Alipoulizwa ana furaha kiasi gani tangu alipojiunga na Inter Miami, Messi alisema: “Nina furaha kwa sababu kuna mechi ya fainali ambayo itaendeleza furaha yangu zaidi.
Nilichagua kuja hapa na ulikuwa uamuzi ambao tulifanya kwa wakati. Hatukufanya uamuzi huu kwa haraka, nilifikiria ndio maana mambo yakaenda sawa pande zote mbili.“