Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi: Ni Kombe la Dunia la mwisho kwangu

Lionel Messi Last Last Lionel Messi

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Argentina Lionel Messi anaamini kuwa mchezo wa Jumapili wa fainali ya Kombe la Dunia Qatar utakuwa mchezo wa mwisho wa kuichezea Argentina Kombe la Dunia.

Maneno ya Lionel Messi mwenye miaka 35 yanakuja baada ya kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kufuzu fainali za Kombe la Dunia linaloendelea Qatar huku ikitegemea kucheza na timu moja wapo kati ya Morocco ama Ufaransa.

Kwenye nusu fainali dhidi ya Croatia iliyopigwa Jumanne, Messi alifunga bao moja na kutengeneza bao la tatu huku mshambuliaji wa Manchester City Alvarez akifunga mabao mawili kwenye ushindi wa jumla ya goli 3-0.

Messi amesema hatagemei kama atacheza fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya sita mpaka sasa ameshiriki mara tano akishindwa kubeba hata mara moja ingawa 2014 alifika fainali na kupoteza kwa Ujerumani.

“Kuna miaka mingi sana kutoka mwaka huu mpaka fainali nyingine, sidhani kama nitaweza kucheza fainali zijazo. Kumaliza fainali hizi vizuri ni jambo kubwa sana”, alisema Messi ambaye kwa sasa anakipiga Paris St-Germain ya Ufaransa ngazi ya klabu.

Messi anakuwa mchezaji wa sita kucheza mashindano ya Kombe la Dunia angalau mara tano wachezaji wengine ni Antonio Carbajal, Lothar Matthaus, Rafa Marquez, Andres Guardado, na Cristiano Ronaldo wa Ureno.

Alipoulizwa yapi mategemeo yao kwenye mechi ya fainali, Lionel Messi mwenye mabao matano na usaidizi wa goli tatu alisema;

“Mategemeo yetu kama timu ni kuona tunashinda mchezo wa fainali. Tutafanya kila linalowezekana uwanjani tushinde kama ambavyo tumekuwa tukifanya kuanzia mwanzoni”, alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live