Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja wa Manula: Diarra ni bora kuliko Aishi, ukweli usemwe

Manula Diarra Mzs Manula na Diarra.

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EFM, Jemedari Said amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 10 (2014-2024) hajawahi kutokea kipa bora kama kipa wa sasa wa Klabu ya yanga, Djigui Diarra raia wa Mali.

Jemedari ambaye pia ni meneja wa kipa wa Simba, Aishi Manula amesema kuwa hata Manula mwenyewe licha ya ubora anaosifiwa nao au kiwango bora kabisa alichowahi kuwa nacho kabla ya kuumia, hajafikia ubora wa Diarra.

“Twende kwenye hizi timu kubwa tatu ndani ya miaka 10, nazungumiza eneo la kipa, hakujakuwa na kipa bora kama Djigui Diarra kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Msimu wa 2013/14 mimi nilikuwa meneja wa Azam FC, kipa wetu alikuwa mwadini, akaondoka akashika Aishi Manula mechi saba za mwisho. Kipa wa Simba alikuwa Abel Dhaira.

“Usajili bora ambao Yanga wameufanya wakati wakitafuta kikombe na mpaka baada ya kuchukua ubingwa ni goalkeeper. Maisha yote ya soka ya Aishi Manula hajawahi kuwa kama Diarra, kwa miaka hii mitatu tatu Diarra aje Bongo, Diarra ni bora na Manula anacheza ligi.

“Jamani tunapaswa kuwa wakweli kwenye jambo linalotaka ukweli. Wakati anakuja Diarra, Aishi alicheza mpaka ligi inaisha, akacheza msimu uliopita akaumia mechi ya Ihefu, akaja msimu huu ndio amecheza nusu nusu lakini Diarra yuko pale na amechukua tuzo ya Kipa Bora kutoka kwa Manula aliyekuwa ametawala miaka ya nyuma.

“Diarra amechukua tuzo mbele ya manula tena bila mtu wa kusema maneno maneno. Msimu huu hata kama Manula mwanangu asingeumia, unaweza ukawaweka kwenye level moja? Jibu ni hapana.

“Mimi Manula sio meneja tu, ni mwanangu kabisa lakini ni ukweli na lazima uwe mkweli. Watu wajue nikisema hiki sicho sio kwa sababu nakuchukia bali kwa sababu namanisha.

“Soka ni Sanaa na ni uwezo wa kuifanya Sanaa yenyewe kwanza ya kucheza mpira kisha ubora wa timu unakuja baadaye. Kuna mtu ana mashaka na Diarra anavyocheza mechi? Hayupo. Uwezo wake yeye akiwa uwanjani?" ameongeza Jemedari Said.

Manula amewahi kuchukua tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu kwa miaka mitano mfululizo lakini tangu Diarra atue nchini, amekomba tuzo hiyo miaka yote miwili na mwaka huu huenda akabeba tena kwani mpaka sasa anaongoza kwa cleansheets huku akiisaidia timu yake kubeba ubingwa na kufika hatua nzuri kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live