Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja wa Kibu afunguka kila kitu

Kibu Denis Prosper Meneja wa Kibu afunguka kila kitu

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetuma ofa kwa uongozi wa mchezaji Kibu Denis ambaye amebakiza mkataba wa mwezi mmoja Simba SC.

Winga huyo mpaka sasa hajaongeza mkataba mpya Simba SC licha ya uongozi wa Simba kumfuata mara kadhaa kumsihi asaini mkataba mpya kuendelea kuwatumikia.

Kibu anadaiwa kuwa amekuwa akiwazungusha viongozi kwamba atasaini tu kwa miezi kadhaa sasa.

Akizungumza hilo, Meneja wa Kibu Denis, Carlos Sylvester amesema; "Ni kweli mteja wangu amebakiza mwezi mmoja Simba. Tumepokea ofa mbalimbali kutoka Norway na Africa.

"Signing fee lazima iendane na mshahara, huwezi kutoa signing fee milioni 300 halafu mshahara uwe milioni 2," amesema Carlos.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live