Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja afunguka: Kibu, Simba lolote linaweza kutokea

Kibu D Hersi Try Again Carlos Slyvester na Try Again.

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa mchezaji wa Simba SC, Kibu Denis aitwaye Carlos Slyvester amesema kuwa sakata la mchezaji wake na Klabu hiyo lolote linaweza kutokea.

Kibu yupo kwenye mazungumzo na klabu yake hiyo kutaka kuongeza mkataba licha ya taarifa kusambaa kuwa amegoma akitaba aongezewe maslahi.

"Ni kweli nimepokea ofa kutoka Simba SC na Young Africans, ninaendelea kuzifanyia kazi, timu ambayo itafikia maslahi basi itafanikisha saini ya mteja wangu ingawa lolote linaweza kutokea.

"Kwa pande zote mbili Simba SC na Young Africans mazungumzo yapo na yanaendelea vizuri, pia sio ofa hizo tu, zipo nyingine kutoka nje ya Tanzania lakini hatuwezi kuweka wazi kwa sasa.

"Kwa timu zote mbili bado makubaliano hayajafikiwa mambo yakienda sawa moja kati ya timu hizo kila kitu kitawekwa wazi mtafahamu kwani mchezo wanaocheza wachezaji ni wa wazi," amesema Carlos Slyvester.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live