Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja: Simba wanamsumbua Mwamnyeto

Mwamnyeto Simba Meneja: Simba wanamsumbua Mwamnyeto

Mon, 18 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MENEJA wa Mchezaji wa Yanga Bakari Mwamnyeto aitwaye Kassa Mussa amedai Klabu ya Simba inamsumbua sana juu ya uwezekano wa kumsajili Mteja wake ambaye ni mchezaji na nahondha wa klabu ya Yanga Bakari Mwamnyeto.

Mussa amesema kuwa Simba wameweka mezani ofa kubwa mno ya kutaka kumsajili mchezaji huyo na mbali na Simba Mwamnyeto amepata ofa nyingine zaidi ya tatu kutoka mataifa ya Ugiriki na Malta.

“Simba wanasumbua sana nisiseme uongo, wamekuwa wakiibuka na ofa kubwa kubwa, ofa yao ni kubwa hasa ambayo nayo tumeamua kuichukua na kuendelea kuifanyia kazi.

“Ukiacha Simba, Bakari ana ofa nyingi sana, kuna ofa tatu au nne hivi, kuna klabu ya Ugiriki, Malta na nyingine moja bado tunazungumza nazo.” Alisema Meneja wa Bakari Nondo Mwamnyeto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live