Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja Pioli kuondoka AC Milan baada ya miaka mitano

Meneja Pioli Kuondoka AC Milan Baada Ya Miaka Mitano Meneja Pioli kuondoka AC Milan baada ya miaka mitano

Fri, 24 May 2024 Chanzo: Bbc

Meneja wa AC Milan Stefano Pioli anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kukamilika.

Mchezo wa mwisho kwa Muitaliano huyo, ambaye amekuwa meneja wa Milan tangu 2019, utakuwa mchezo wa Jumamosi wa Serie A dhidi ya Salernitana.

Pioli aliiongoza Milan kutwaa taji lao la kwanza la Serie A katika kipindi cha miaka 11 mnamo 2022.

Walimaliza katika nafasi ya nne msimu uliofuata lakini bodi ilikuwa na imani na Pioli baada ya Milan kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, ambapo walitupwa nje na wapinzani wao wa ndani Inter Milan.

AC Milan wana uhakika wa kumaliza nafasi ya pili kwenye Serie A msimu huu lakini wanaingia katika raundi ya mwisho ya mechi Jumamosi wakiwa pointi 19 nyuma ya mabingwa Inter.

Mkataba wa Pioli ulikuwa unamalizika 2025, lakini pande zote mbili zimekubali kusitisha mkataba wake sasa. AC Milan walitoa "shukrani zao za dhati" kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 58 na kusema alisaidia "kuifufua tena" klabu hiyo kama nguvu ya Ulaya.

Chanzo: Bbc