Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja Leicester City afukuzwa kisa mahusiano na Mchezaji

Meneja Leic Klabu ya Leicester City ya wanawake imemfukuza kazi meneja wake Willie Kirk

Fri, 29 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Leicester City ya wanawake imemfukuza kazi meneja wake Willie Kirk kufuatia uchunguzi kuhusiana na tuhuma kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji.

Kirk, 45, alisimamishwa kazi na klabu hiyo inayocheza Ligi Kuu ya Wanawake ya England, WSL mapema mwezi huu “ili kusaidia uchunguzi wa ndani”.

Meneja huyo anayetokea Scotland, hakuwepo uwanjani kusimamia mechi tatu zilizopita.

“Willie ameonekana kukiuka kanuni za timu kiasi kwamba kuwepo kwake hakuwezi kuendelea,” imesema taarifa ya Leicester.

Malalamiko yaliwasilishwa kwa klabu hiyo kufuatia kuwepo na tuhuma za uhusiano wa kimapenzi kati ya Kirk na mchezaji wa timu hiyo imesema BBC Sport.

Uhusiano wa kocha na mchezaji sio kuvunja sheria, ikiwa hakuna watoto waliohusika, lakini hali hiyo inaweza kuvunja kanuni.

Kanuni zilizopo miongoni mwa wachezaji na mameneja katika soka la wanawake ni kigezo cha kupata leseni ya kucheza Ligi ya WSL na kila klabu lazima iwe na afisa msimamizi wa kuhakikisha kanuni zinasimamiwa.

Uhusiano wa wachezaji na mameneja umeshutumiwa katika soka la wanawake kwa kuweka uwezekano wa timu kukosa uwiano. KÐ

Chanzo: www.tanzaniaweb.live