Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mendy kuongeza Mkataba Chelsea mpaka 2025

Mendy Chelsea Mlinda mlango wa Chelsea, Eduardo Mendy

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Chelsea inaanda mkataba mpya kwaajili ya Golikipa wake msenegali Edouard Mendy baada ya kuonyesha kiwango kikubwa na kuisaidia timu hiyo kutwa Klabu Bingwa Barani Ulaya.

Mendy, 29 anatarajiwa kusaini mkataba mpya ulioongezwa mshahara na marupurupu ikiwa ni mwaka mmoja tangu ajiunge na Chelsea akitokea Rennes ya Ufaransa kwa dau la £22 million.

Kipa huyo alisaini mkataba wa miaka 5 mwaka 2020 ambao ulimfanya alipwe kiasi cha Pauniu elfu 60,000 kwa wiki na sasa Chelsea wanataka kuboresha mkataba wake baada ya kufanya vizuri klabuni hapo.

Mendy amefanikiwa kuweka Cleansheet 36 katika mechi 63 alizocheza tangu ajiunge na miamba hiyo ya London, huku msimu huu akiruhusu magoli 6 pekee katika mechi 13 alizocheza akiwa hajaruruhusu wavu wake kuguswa mara 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live