Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mendy awabwaga Mane, Sarr Senegal

2910748 59827968 2560 1440 Edouard Mendy

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango wa Chelsea, Edouard Mendy, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Senegal, ambayo hutokana na kura za waandishi wa habari nchini humo.

Mendy ameibeba tuzo hiyo akiwapiku wakali wengine wanaokipiga Ligi Kuu England; Sadio Mane (Liverpool) na Ismaila Sarr (Watford).

Ukiwa ni mwezi mmoja umebaki kabla ya kuanza kwa fainali za Afcon, kipa huyo ameibuka kidedea baada ya kujikusanyia kura 321, akifuatiwa na Mane (99) na Sarr (61).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live