Benjamin Mendy anatarajia kuishitaki klabu ya Man City kwa kutokumlipa kuanzia Agosti 2021 hadi June 2023, Mendy inadaiwa kuwa anaidai klabu hiyo ya Man City Zaidi ya Euro Milioni 11.5.
Mendy anasema kipindi cha matatizo Man City ilimterekeza na ilikuwa haimlipi pesa ya mkataba.
Mlinzi huyo wa zamani wa Manchester City, baada ya kusota mahabusu kwa zaidi ya mwaka, hivi karibuni alikutwa hana hatia ya katika mashitaka mawili yaliyokuwa yakimkabili moja la ubakaji na lingine la kujaribu kubaka.
Ikiumbukwe mnamo Januari Mfaransa huyo alikutwa hana hatia ya makosa sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono dhidi ya wasichana wanne ambapo alibakiwa na makosa mawili ya kubaka na kujaribu kubaka ambayo leo yamefutwa yote.
Mendy na rafiki yake Matturie, walishtakiwa karika mahakama ya Chester Crown kwa kubaka wanawake katika nyumba ya mchezaji huyo huko Prestbury, Cheshire na kukana mashitaka hayo kwa madai matukio hayo yalikuwa ya makubaliano.
Mendy alijiunga na Manchester City mnamo mwaka 2017 kutoka klabu ya AS Monaco kwa ada ya takriban $68m. Alikabiliwa na uchunguzi wa polisi baada ya wanawake 13 kutoa tuhuma dhidi yake na mshitakiwa mwenza Louis Saha Matturie.
Mendy baada ya kurejea uraiano ameshasaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia klabu ya Lorient inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa (Ligue 1).