Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mendy, ashangazwa kukosekana kwenye Ballon d'Or

Tanazania 1024x705 Edouard Mendy

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Golikipa wa Chelsea Edouard Mendy ameshangazwa kutoorodheshwa kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa ulaya Ballon d'Or. Anahisi kutoichezea timu ya taifa ya Ufaransa inaweza kuwa ni moja ya sababu ya kutojumuhishwa, tuzo hiyo itatolewa November 29, 2021.

Mendy Mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Chelsea msimu uliopita kwa mkataba wa miaka 5 akitokea katika klabu ya Rennes ya Ufaransa na alikuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kilichotwaa ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya Msimu uliopita na kuweka rekodi yakuwa golikipa wa kwanza mweusi kutwaa ubngwa huo wa vilabu barani ulaya.

"Kama ningekuwa naichezea timu ya taifa ya Ufaransa na ningekuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa ulaya, tungekuwa na huu mjadala? Nadhani hii sio haki? Hapana siwezi kutumia neno hilo, lakini hii imenifanya nizidi kupambana na kusonga mbele, nifanye kazi zaidi ili niwe kwenye kiwango bora kwa klabu yangu na timu yangu ya taifa". Amesema Mendy alipoulizwa kwa kutoorodhesha kwake kwenye tuzo hiyo.

Golikipa huyo ni mzaliwa wa Montivilliers Ufaransa lakini akachagua kuichezea timu ya taifa ya Senegal. Licha ya yeye kutoorodheswa lakini Chelsea imetoa wachezaji watano (5) wanaowania tuzo hiyo ambao ni Jorginho, Cesar Azpilicueta, Mason Mount, N'Golo Kante na striker Romelu Lukaku.  

Chanzo: eatv.tv