Thu, 11 Aug 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Beki wa kushoto wa Manchester City Benjamin Mendy ameendelea kukanusha tuhuma za kuhusika na kitendo cha ubakaji.
Mahakama ya Chester Crown ndiyo ilikuwa inasikiliza tuhuma hizo ambazo zinaelekezwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa Monaco ambapo mpaka sasa amepinga mashitaka manane.
Baadhi ya mashataka hayo ni kuwa, Mendy mwenye umri wa miaka 28 alitaka kubaka na kwa matumizi ya nguvu dhidi ya mpenzi wake pamoja na jaribio la kubaka.
Mchezaji huyo ambaye kabla ya kusimamishwa na klabu yake ya Manchester City alikuwa amecheza jumla ya mechi 50 tangia mwaka 2017.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live