Kipa wa kimataifa wa Senegal Edouard Mendy, 31, ameambiwa anaweza kuondoka Chelsea dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa atapata timu itakayokuwa tayari kumnunua.
Mara kadhaa Mendy alikataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Chelsea kwa sababu ofa iyowekwa mezani ilikuwa ni ndogo kuliko kile anachokihitaji.
Kwa sasa Chelsea inaonekana kumtumia zaidi kipa wao Kepa Arrizabalaga badala yake imeripotiwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kumsajili kipa mpya ili kuziba pengo la Mendy ikiwa ataondoka.
Mendy mara kadhaa aliripotiwa anahitaji mshahara usiopungua Pauni 170,000 kwa wiki ambao ndio mshahara wa sasa wa Kepa.