Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mendy akiri kufanya ngono na wanawake elfu kumi

Mendy Akiri Kufanya Ngono Na Wanawake Elfu Kumi Mendy akiri kufanya ngono na wanawake elfu kumi

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: Wasafi FM

Mwanasoka wa Manchester City, Benjamin Mendy (28) anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka 28 na kumwambia msichana huyo “ni sawa, kwani ameshafanya ngono na wanawake 10,000”.

Mendy anatuhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, wakiwa kwenye jumba lake la kifahari huko Mottram St Andrew, Cheshire, Oktoba 2020.

Aidha, anatuhumiwa kwa jaribio la kumbaka msichana mwingine, mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia alimshambulia nyumbani kwake miaka miwili iliyopita.

Baada ya kusomewa mashtaka yote mawili katika Mahakama ya Chester na Jaji Stephen Everett, mwanasoka huyo alikanusha kuwa hakufanya makosa hayo.

Chanzo: Wasafi FM