Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mendes alazimisha Nunez aende Barcelona

Darwin Nunez3 1200x630 Darwin Nunez

Sat, 11 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakala wa Darwin Nunez, Jorge Mendes ameripotiwa kufichua kile ambacho Liverpool inataka ilipwe wakati huu akijaribu kupambana mteja wake aende kujiunga na Barcelona.

Kinachoelezwa ni kwamba Barca inapiga hesabu za kumchukua Nunez ili akachukue mikoba ya straika Robert Lewandowski.

Na fowadi huyo wa kimataifa wa Uruguay, Nunez ameibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufuta picha zake zote zinazojihusisha na Liverpool kwenye ukurasa wake wa Instagram. Na alionekana Barcelona siku ya mapumziko ya mazoezi huko Liverpool.

Kwa mujibu wa taarifa za kutoka Hispania, wakala wa Nunez, Jorge Mendes anafanya kila analoweza kuhakikisha dili hilo linatiki.

Na kinachoelezwa, wakala huyo amewaambia Barcelona, kwamba Liverpool itakubali kupokea ofa ya Pauni 73 milioni kwenye mauzo ya mshambuliaji huyo.

Na Barca, ambayo kwa sasa ina matatizo ya kifedha, inaamini itaweza kulipa ada hiyo kama tu itapiga bei baadhi ya mastaa wake wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Kinachotishia ni kwamba Barcelona imepangiwa mshahara wake usizidi sana Pauni 174 milioni, hivyo ni lazima ipige bei mastaa wake ili kujijenga upya.

Msahahara wa Lewandowski kwenye kikosi hicho unaripotiwa utafika Pauni 27 milioni kuanzia msimu ujao, hivyo wanapambana kuhakikisha wanampiga bei dirisha lijalo la usajili.

Chanzo: Mwanaspoti