Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Medo aichorea ramani Yanga

Medo Pic Data Medo aichorea ramani Yanga

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mzuka umeanza kurejea kwa Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji Mmarekani, Melis Medo baada ya kutamba kuendeleza wimbi la ushindi wakati timu yake itakapokuwa na kazi ngumu ya kuidhibiti Yanga kesho Jumanne kwenye Uwanja wa Liti Singida.

Akizungumza Medo aliyewahi kuzifundisha timu za Coastal Union na Gwambina kwa nyakati tofauti tofauti alisema licha ya kutegemea mchezo mgumu kutoka kwa wapinzani wao ila matumaini yake ni kupata pointi tatu.

"Ushindi wa 2-1 dhidi ya KMC mchezo uliopita umetuongezea morali na hali ya kujiamini kwa wachezaji wangu hivyo jukumu pekee ni kuendeleza kiwango bora tulichokionyesha ingawa tutakutana na ushindani mkubwa."

Medo aliongeza pamoja na hilo ila bado ana kazi kubwa ya kufanya eneo la ulinzi kwani limekuwa na shida kubwa msimu huu kutokana na wao kuruhusu idadi kubwa ya mabao 15 tofauti na yaliyofungwa na timu nzima saba (7).

Tangu Medo amekabidhiwa timu hiyo Oktoba 11 mwaka huu ameongoza katika michezo mitano na kati ya hiyo ameshinda mmoja tu na KMC (2-1), akifungwa mitatu (2-0) na Ihefu, (1-0) na Mtibwa Sugar, (2-1) na Azam kisha sare ya 1-1 na Polisi Tanzania.

Wakati Medo akiyasema hayo haitokuwa rahisi kwake kucheza na Yanga ambayo imekuwa kwenye kiwango kizuri huku mara ya mwisho kwao kupoteza katika Ligi Kuu Bara ilikuwa Aprili 25, mwaka jana ilipofungwa bao 1-0 na Azam.

Mbali na hilo, Dodoma Jiji tangu ipande rasmi Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 haijawahi kuifunga Yanga kwani katika michezo minne waliyokutana imefungwa mitatu na sare moja huku mara ya mwisho ikifungwa 2-0 Mei 15 mwaka huu.

Medo alichukua nafasi ya Masoud Djuma aliyeachana na timu hiyo Oktoba 10 kutokana na matokeo mabovu ambapo alifanikiwa kukiongoza michezo sita ikishinda mechi moja, akitoa sare miwili na kupoteza mitatu.

Kwa upande wa mshambuliaji wa timu hiyo ambaye ndiye kinara wa mabao akiwa na matatu Mghana, Collins Opare alisema licha ya kutokuwa na matokeo mazuri mfululizo ila anaamini mchezo wao na Yanga wana uwezo wa kufanya vizuri.

Chanzo: Mwanaspoti