Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Medo aanza kunogewa Bara

Medo Pic Medo aanza kunogewa Bara

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya ya Coastal Union, umempa jeuri Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Mmarekani Melis Medo aliyetamba kuanza kupata mwanga wa kurejesha morali ya timu hiyo iliyoanza msimu vibaya.

Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Mkwakwani shujaa aliyeipatia timu hiyo pointi tatu ni Rashid Chambo aliyepiga shuti kali dakika ya 89 na kumshinda kipa Mahamoud Mroivili.

Akizungumza Medo alisema ushindi huo ni njia ya kuwarejesha kwenye mstari ingawa bado ana kazi kubwa ya kufanya hususan katika eneo la ulinzi na ushambuliaji.

“Tunatengeneza nafasi nyingi ila bado tunashindwa kuzitumia vizuri, muunganiko sio mzuri japo kikubwa kwa sasa ni kupata pointi tatu kwenye kila mchezo,” alisema na kuongeza;

“Muda mwingine tunapoteza kwa sababu ya matokeo ya mpira ila haina maana timu haichezi vizuri, tuna muda wa kurekebisha changamoto zilizopo ili kutufanya tuwe bora zaidi ya hapa.”

Tangu Medo amekabidhiwa kikosi hicho Oktoba 11 amekiongoza katika michezo minane na kati ya hiyo ameshinda miwili, sare mmoja na kufungwa mitano kikishika nafasi ya 13 na pointi 12. Medo alichukua nafasi ya Masoud Djuma aliyeachana na timu hiyo Oktoba 10, kutokana na matokeo mabovu ambapo amekiongoza katika michezo sita, akishinda mmoja, sare miwili na kupoteza mitatu.

Chanzo: Mwanaspoti