Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Medeama yawapiga wababe wa Yanga

Medeama 524 Medeama yawapiga wababe wa Yanga

Sat, 2 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Ghana, Medeama SC wamefanikiwa kuibuka na alama tatu baada ya kuifunga CR Belouizdad ya Algeria bao 2-1 jioni ya jana.

Mchezo huo wa mkondo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ulipigwa katika Dimba la Baba Yara Sports Stadium nchini Ghana.

Belouizdad ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Benguit dakika ya 39' kwa mkwaju wa penati.

Baadaye Medeama walifanya comeback ya kibabe na kusawadhisha bao hilo kupitia kwa Lomotey dakika ya 45' kabla ya Mamudu Kamaradin kupigilia msumari wa pili dakika za nyongeza 90+4' na kuwafanya Waarabu waondoke mikono mitupu.

Medeama ambao wanatajwa kama vibonde kwenye kundi hilo, wameupiga mpira mwingi ambao hata Waarabu hawakutegemea.

Takwimu za mchezo

Medeama SC -------------- CR Belouizdad

18------------ Shots-----------6

5-------Shots on target--------3

61%--------Possession---------39%

355-----------Passes----------243

82%-------Pass accuracy-------71%

16------------Fouls------------29

1---------Yellow cards----------7

0-----------Red cards-----------0

3------------Offsides----------01

1-------------Corners-----------2

Vikosi vya timu zote

Medeama FC 4-3-3

F. Kyei

K. Amoako

N. Abdulai

E. Cudjoe

Mamudu Kamaradin

M. Mantey

B. A. Musah

J. V. Ourega

D. Lomotey

J. Agyemang

D. Fordjour

CR Belouizdad 4-3-3

A. Guendouz

M. Belkhiter

C. Keddad

M. Hadded

Y. Laouafi

H. Selmi

M. Samake

A. Benguit

I. Boussouf

O. Darfalou

A. Meziane.

Ikumbukwe kuwa, CR Belouizdad wakiwa nyumbani kwao nchini Algeria waliifunga Yanga kwa mabao 3-0, wakati Al Ahly wakiifunga Medeama kwa mabao 3-0. Hivyo katika kundi hilo kwa sasa Yanga pekee ndiyo hana alama hata moja wakati timu nyingine zikiwa na alama 3 kila mmoja.

Leo Jumamosi, Desemba 2, 2023 katika Dimba la Mkapa, Yanga watavaana na Al Ahly katika mchezo wa raundi ya pili ya hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live