Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Medeama wazipigia hesabu alama tatu za Yanga

Medeama FC Point 3 Medeama wazipigia hesabu alama tatu za Yanga

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya Mitandao mbalimbali ya michezo hapa Ghana, imeripoti taarifa mbalimbali kuelekea mchezo wa Ijumaa Desemba 8, Medeama SC dhidi ya Yanga SC, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Baba Yara Sports Stadium.

Mitandao mingi imeripoti namna ambavyo Rais wa Medeama SC, Moses Armah Parker amekuwa na matumaini ya timu yake kufuzu robo fainali ya CAF Champions League mara baada kushinda mchezo wao dhidi ya CR BELOUIZDAD.

Rais Moses Armah Parker anasema kushinda kwao mchezo dhidi ya CR Belouizdad umezindua matumaini ya wao kufuzu hatua ya mtoano kama watashinda michezo yao ya nyumbani, amesema wataanza na mchezo dhidi ya Yanga SC ijumaa hii.

Kuna mtandao mwingine imeripoti namna ambavyo Yanga SC imewasili Jana, Accra na hapo hapo kuunganisha ndege hadi Kumasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live