Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Medeama wakiamua kukushughulikia ni hatari - Luambano

Medeama Msled Medeama wakiamua kukushughulikia ni hatari - Luambano

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa habari za michezo kupitia Clouds FM, Alex Luambano amesema kuwa Klabu ya Yanga wanapaswa wafanye kazi kubwa ugenini kuwadhibiti Medeama FC kwani timu hiyo licha ya wengi kuwachukulia kama wanyonge, lakini wakiamua kupiga soka Wananchi watakuwa kwenye wakati mgumu.

Luambano amesema hayo kupitia Hill Game ya Clouds FM kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Medeama na Yanga utakaopigwa huo Kumasi nchini Ghana kesho.

“Kesho Yanga wanashuka uwanjani ugenini, ni mechi nyingine ngumu ingawa makundi yalipopangwa ilionekana kama itakuwa mechi ya kawaida, makundi yalipotoka mechi ya Medeama na Yanga ilikuwa inaonekana itakuwa mechi nyepesi.

“Lakini mpaka sasa hivi na hii ni moja ya mechi ngumu pia, sio mechi nyepesi kwa Yanga, kwa kile walichokionesha Medeama kwa mechi hizi mbili, wamempiga Belouizdad, walifungwa na Al Ahly lakini Ahly walishika bomba (waliteseka).

“Wakiamua kushika bomba wanaweza kushikilia, wakiamua kukushughulikia wanaweza, lakini Yanga nao sio timu dhaifu mbele ya Medeama," amesema Luambano.

Mechi itachezwa kesho, hadi muda huu unaipa timu ipi nafasi ya kushinda hii game?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live