Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mecky Mexime na somo la kujitambua kwa Makocha wazawa

Mecky Maxime Best Coach Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika nyakati ambapo kumejengwa dhana ya makocha wazawa kuchukuliwa poa, Mecky Maxime yeye amejichorea kieneo cha peke yake.

Hajakubali unyonge mbele ya makocha wa kigeni ambao ndio wamekuwa wakipewa thamani kubwa kuliko wazawa.

Hivi unavyosoma andiko hili, Mecky Maxime ni miongoni mwa makocha wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha kama mshahara katika Ligi Kuu.

Amejitambua thamani yake na ameamua kuilinda kwa nguvu zote ili iendeshe vizuri maisha yake.

Anajua katumia gharama kubwa ya fedha kupata elimu yake hivyo hakubali idharaulike kirahisi kwa kulipwa kiduchu kiufupi hajakubali kuwa mtu rahisi rahisi.

Kocha ambaye ameweka sharti kwa hizo timu kubwa kuwa kama zinamhitaji basi zikubali awe kocha mkuu na kocha mzungu au wa kigeni awe msaidizi kwake.

Alikuwa nahodha wa kikosi dume cha Mtibwa Sugar kikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo.

Amekuwa nahodha wa Taifa Stars aliyeagwa kwa heshima.

Mecky Maxime anaweza asikufurahishe kwa maneno yake iwapo umemuingia kichwakichwa lakini anabakia kuwa miongoni mwa makocha wachache wazawa wanajua kusimamia misimamo na taaluma zao

Chanzo: www.tanzaniaweb.live