Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mecky Mexime: Hao Yanga msimu ujao, mhhh...!

Yanga Vs Augusburg Mecky Mexime: Hao Yanga msimu ujao, mhhh...!

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Mecky Mexime amesema kuwa Ligi Kuu msimu ujao itakuwa ngumu kutokana na usajili uliofanywa na vilabu vyote vinavyoshiriki ligi hiyo.

Meccky ambaye amewahi kuifundisha Ihefu FC msimu uliopita amesema hayo wakati akiongea na Efm radio huku akidai kuwa usajili uliofanywa na Yanga ni mzuri zaidi kuliko vilabu vingine ndani ya ligi.

"Msimu ujao ligi itakuwa nguma zaidi kwa sababu timu zimeboresha vikosi vyao, hasa Yanga. Yanga tayari wanakikosi kizuri lakini wameboresha kwa kufanya usajili.

"Duke Abuya nimemfundisha pale Ihefu, naweza kusema Abuya ndio usajili bora zaidi wa Yanga dirisha hili, ni mchezaji bora aliyekamilika ambaye kila mwalimu angetamani kuwa na mchezaji kama huyo kwa sababu anakupa kila kitu unachohitaji.

"Hajaimbwa sana lakini nauhakika ataimbwa sana ligi itakapoanza," amesema Kocha Mecky Mexime.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live