Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mecky Maxime awaamsha wazawa Bara

Aswrw Mecky Maxime awaamsha wazawa Bara

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Dodoma Jiji, Mecky Maxime ameamsha wachezaji wazawa kwa kuwataka wapambane ili kupata nafasi katika timu wanazozitumikia, hasa nyakati hizi ambazo kuna ushindani dhidi ya nyota wa kigeni.

Maxime anayeendelea na kambi ya maandalizi (pre season) jijini hapa, kuhakikisha msimu mpya wa Ligi 2024/25 timu yake inafanya vizuri Ligi Kuu na Kombe la FA, aliliambia Mwanaspoti kutokana na ushindani mkubwa uliopo sasa hivi kwenye Ligi kila timu inatafuta mchezaji gani ambaye anaweza akampa matokeo na wala sio kuangalia huyu ni mzawa.

“Ukienda timu zote za Ligi Kuu zina wachezaji wa kigeni na wengine zaidi ya 10, vijana wetu wakipata nafasi sasa hivi ya Ligi Kuu wajishike miaka inavyokwenda hivi wengi watapungua,” alisema nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Taifa Stars.

"Mchezaji akija kwangu anakuja kunisaidia, akileta mizinguo nampotezea kwani kuna wanaoridhika mara wanaposajiliwa na hilo ni jambo baya na linachochangia sana kufukuzisha makocha, mie nataka mtu wa kupambana na kokote walipo wapambane wasibweteke," aliongeza Maxime.

Aliweka wazi kuwa hata wao makocha wanapopata nafasi timu zinawaamini wanakaza kufundisha na kuonyesha kile kitu ambacho hata watu wa pembeni wanaona kabisa hii timu ina mwalimu na kushawishi waajiri wengine.

Chanzo: Mwanaspoti