Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Mechi za kirafiki zisiwadanganye’

Victor Osimhen Nigeria ‘Mechi za kirafiki zisiwadanganye’

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nigeria iko nusu fainali ya Mataifa ya Afrika licha ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha ya mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 na zile za kirafiki za kujiandaa na Afcon.

Katika mechi yao ya mwisho kabla ya kwenda Ivory Coast, Super Eagles walilala 2-0 dhidi ya Guinea na kushindwa kupata ushindi mbele ya Saudi Arabia wakitoka 2-2 katika mechi ya kirafiki.

“Mechi ya kirafiki kwangu mimi ni ya kuangalia na kujaribu vitu fulani. Nimekuwa nikizitumia mechi za kirafiki kuwajaribu wachezaji dhidi ya timu tofauti. Na kwa kuwa tulicheza mechi nyingi za ugenini, hii pia ilikuwa ni sababu. Nigeria ilicheza mechi za kirafiki ugenini dhidi ya Ureno, Mexico na Msumbiji, kwangu mimi mechi za kirafiki ni kwa ajili ya mazoezi na kuangalia mambo fulani,” alisema kocha mkuu wa Nigeria, Jose Peseiro.

Licha ya Super Eagles kuwa na mabao machache wakifunga sita tu katika mechi tano kwenye Afcon, wamepaa hadi nusu fainali, na kocha mkuu Peseiro amesisitiza kwamba mechi zao za kirafiki hazikubeba picha halisi ya utayari wao kwa ajili ya Afcon.

“Ni kweli matokeo ya mechi zetu zilizopita hayakuwa mazuri lakini tuko hapa.”

Chanzo: Mwanaspoti