Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi yamkutanisha na mwizi wa mume wake

Mbagalaaaa 0001 Mechi yamkutanisha na mwizi wa mume wake

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mitaa ya Mbagala haijawahi kupoa kabisa, wiki hii shabiki wa Kwa Mkongo Queens amemkamata aliyemwibia mume wake na kuliamsha.

Wiki iliyopita ilianza michuano ya Chaurembo Rede Cup 2024 na Mkongo ikaanza kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Kilungule Queens, Uwanja wa Shule ya Msingi Chamazi.

Shabiki huyo anayefahamika kwa jina la Mwanahamisi wakati watu wanatazama mechi akaanzisha vurugu na kusema baada ya kusema: “Atanitambua alijua hatutakutana.”

Unaambiwa yule mwizi wa mume wa mtu baada ya kuona Mwanahamisi anamfuata akaona isiwe tabu naye akaanza kutimua mbio kwa kasi.

“Kuna watu wanatuharibia sana furaha yetu. Leo nimekuja uwanjani kufurahi nimemuona mwanamke aliyekuwa ananiibia mume wangu halafu nilivyowakuta alikuwa na jeuri leo mbona amenikimbia,” alisema Mwanahamisi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live