Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya mwisho kuamua Bingwa wa EPL

Arsenal Vs Man City Mechi ya mwisho kuamua Bingwa wa EPL

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sasa ni rasmi bingwa wa ligi kuu soka nchini England ataenda kujulikana kwenye michezo ya mwisho ya ligi hiyo itakayotamatika jumapili Mei 19 baada ya dua za Arsenal kufeli usiku wa kuamkia leo uliomshuhudia 'Jini' Earling Halaand akifunga mabao yote mawili kwenye ushindi muhimu wa 2-0 ugenini walioupata Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur na kurejea kileleni kwenye msimamo wa EPL

City pia wamepunguza wastani wa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kati yake na Arsenal ambapo sasa wanatofautiana bao moja pekee huku wakimuacha Arsenal kwa alama mbili kwenye msimamo

Mchezo wa mwisho City watakuwa nyumbani dhidi ya West Ham United huku Arsenal wakiwakaribisha Everton ambapo miamba hiyo ya London watakuwa na dua mbilimbili za usumbufu kwa Muumba wakiombea wapate ushindi kwenye mchezo wake huku wakati huohuo wakiwaombea City wapoteze kimiujiza nyumbani dhidi ya West Ham United ili waweze kutwaa taji la EPL kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live