Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya jana ilikuwa kipimo kwa wenye matatizo ya presha - Mpenja

Yanga Azam FC 000 Mechi ya jana ilikuwa kipimo kwa wenye matatizo ya presha - Mpenja

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anaandika Baraka Mpenja NAFIKIRI SASA WATU WENGI MMEELEWA KWAMBA MNA PRESHA....lakini kama hamkufa jana katika hatua ya Mikwaju ya penati Uwanja wa Amaan Zanzibar, basi mtaishi sana, Dadadadadadeki!

Mwezi wa Tisa mwaka huu, In Nsha Allah, nitatimiza miaka 10 ya Utumishi ndani ya Azam Media LTD na katika kipindi hiki chote nimetangaza mechi nyingi kubwa zikiwemo FAINALI, lakini FAINALI ya jana ya CRDB Bank Federation Cup kati ya AZAM FC VS YANGA...ilikuwa ya miujiza na ndoto za kutisha.

Dakika 120' bora, kisha penati 18 zilipigwa, tisa tisa kwa kila timu, final score, Azam Penati 5, Yanga 6.

Zile moments za Yanga kukosa penati mbili za mwanzo na kisha mambo kukaa baadaye, nilishuhudia Watu wengi wakitetemeka mno kwa hofu, nyuso zilijaa huzuni na wasiwasi wa kutisha.

Baada ya penati tano za kwanza na timu kuwa mzani sawa, Azam FC ilipata Penati mbili za kushinda Fainali, lakini WALIKOSA, hakika hofu ilitanda kwa YANGA.

Wananchi Waliposhinda PENATI, wengi walichanganyikiwa na kulia kwa furaha, ulikuwa usiku wa miujiza, usiku wa kukumbukwa ukitangazwa na MWAMBA WA UMALILA.

Nimefurahi kuwa MTANGAZAJI wa Fainali hii kubwa na bora mno mno mnooo! nikiwa na Pacha wangu wa muda mrefu JAMES SAMWEL @james_samwel31

Almost MIAKA 10 natangaza mfululizo, namshukuru Mungu, Familia yangu, Kampuni yangu ya Azam Media kwa kuniamini kwa kipindi chote, lakini pia MASHABIKI wangu wote mnaonisapoti kila wakati.

Bye bye! Msimu wa 2023/2024, let us wait and see msimu mpya MUNGU atatujaalia nini, In Nshaa Allah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live