Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya dabi ni ya kutupa ramani ya ubingwa - Kapombe

Shomari Kapombe Mechi ya dabi ni ya kutupa ramani ya ubingwa - Kapombe

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kulia wa timu ya Simba, Shomari Kapombe amesema kuwa wamejiandaaa vizuri kwa ajili ya mchezo wao wa dabi dhidi ya watani zao yanga SC utakaopigwa kesho Aprili 20 katika Dimba la Mkapa.

Kapombe amesema kuwa malengo yao ni kushinda mchezo huo, hivyo kocha amewaelekeza mambo yote muhimu ya kufanya ili kutoka na ushindi huku akisahihisha makosa ya wachezaji wake ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.

“Mechi ya kesho ndiyo itatupa njia ya kuchukua ubingwa. Ligi ina mechi nyingi, kwa hiyo ni mpaka mchezo wa mwisho ukiisha ndipo utajua bingwa ni nani. Sisi tunaanza mchezo wa kesho kuupambania ubingwa.

“Nawaomba mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi kuja kutusapoti. Tunahitaji sapoti yao sana wasiangalie huko nyuma tumepoteza lakini waje kutupa nguvu. Tunaamini kutokana na maandalizi tuliyofanya kesho tutawapa furaha,” amesema Kapombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live