Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Yanga vs Azam FC yasogezwa mbele tena

Yanga Vs Azam 2 0 FT.jpeg Yanga vs Azam FC.

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC na Azam FC, umesogezwa mbele kutoka kupigwa Jumapili Oktoba 22,2023 na sasa utapigwa siku ya Jumatatu Oktoba 23, 2023 kwenye uwanja wa Azam Comple,Chamazi.

Sababu za kusogezwa mbele kwa mchezo huo zikitajwa ni uwepo wa mchezo wa kimataifa wa African Football League baina ya TP Mazembe dhidi ya Esperance De Tunis, ya Tunisia utakaopigwa siku ya tarehe 22, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.

Aidha, mchezo wa Ligi Kuu kati ya Singida Fountain Gate FC na Yanga SC nao utakaopigwa katika Dimba la Liti mkoani Singida, umesogezwa mbele kutoka Oktoba 26, mpaka Oktoba 27, 2023.

Muda wa mechi za Yanga za ligi kuu katika uwanja wa Azam complex :

Jumatatu Oktoba 23

◉ Yanga vs Azam — Saa 12:30 jioni

Ijumaa Oktoba 27

◉ Yanga vs Singida — Saa 12:30 jioni

Chanzo: www.tanzaniaweb.live