Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Yanga na Azam ni kama birthday tu - Jemedari Said

Jemedari X Yao Mechi ya Yanga na Azam ni kama birthday tu - Jemedari Said

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said amesema kuwa mchezo wa Yanga dhidi ya Azam FC ilikuwa ni lazima usogezwe mbele kupisha michezo ya African Football League (AFL).

Jemedari amesema hayo baada ya mchezo huo uliokuwa umepangwa kufanyika Oktoba 22, 2023 katika Dimba la Azam Complex, kusogezwa mbele siku moja mpaka Oktoba 23, kupisha mchezo wa AFL kati ya TP Mazembe ya Congo Dr dhidi ya Esperance De Tunis ya Tunisia.

"Kwa sasa ukisoma maandiko mbalimbali ya wachambuzi na waandishi tumeamua kujiweka wazi kuhusu klabu tunazoshabikia. Tofauti yetu ni wengine wanaongea facts na ushahidi na wengine wanaongea kwa kuwa mdomo wanao, hawalipii kodi.

"Hapa ilikuwa lazima mechi ya Ligi kuu isogezwe (Yanga na Azam), ni kama Birthday inapoangukia siku ya harusi, Birthday itasogezwa tu mbele harusi ipite.

"Kuna mechi mbili tu Tanzania, Simba, Al Ahly na TP Mazembe na Esperance. Hizo zingine hatuzijui. AFL ndiyo jambo kubwa la soka Afrika kwa sasa na mechi zake ndiyo mechi kubwa za soka kila zitakapochezwa," amesema Jemedari Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live