Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Tanzania vs Morocco inakumbusha kisa cha Achraf Hakimi

Hakimi Ghs 55851272

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unakikumbuka kisa cha mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco na PSG Achraf Hakimi na mkewe Hiba Abouk kudai nusu ya mali za mume wake baada ya kutalakiana.

Mchezaji huyo leo atashuka uwanja wa Benjamin Mkapa na timu yake ya taifa ya Morocco mchezo wa kufuzu kombe la dunia.

Kesi yao ya madai ya talaka ilipelekwa mahakamani Machi 2023 ambapo Bi Hiba alidai kwamba anataka kulipwa pesa na nusu ya mali, lakini baadae ilikuja kufahamika kwamba 80% ya mali za Hakimi zimeandikwa jina la mama yake mzazi.

Kuelekea mchezo huu wa kutafuta tiketi ya kuwania kombe la dunia, akifanya mahojiano na waandishi wa habari Achraf Hakimi alisema kwamba wanafahamu Tanzania ni timu nzuri lakini hata wao ni wazuri na hivyo wataingia uwanjani kupambana kushinda.

Hakimi Achraf na mkewe Hiba Abouk walianza uchumba na mapenzi mwaka 2018 na miaka miwili mbele yaani 2020 walifunga ndoa ya kiislamu ambapo, walijaliwa kupata watoto wawili. Mgogoro wao wanandoa hawa ulikuja baada ya mchezaji huyo kuhusishwa na masuala ya ubakaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live