Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Simba na JKT Tanzania yabadilishwa uwanja

94852 Pic+simba Mechi ya Simba na JKT Tanzania yabadilishwa uwanja

Fri, 7 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

MECHI ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na JKT Tanzania awali ilikuwa ichezwe Uwanja wa Taifa saa 1:00 usiku lakini mapema asubuhi ya leo Ijumaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wamefanya mabadiliko ya mchezo huo ambapo sasa utaanza saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru. Afisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema mchezo huo umebadilishwa muda na uwanja kutokana na kuwepo na matumizi mengine kwenye Uwanja wa Taifa kwa muda unaofanana. Ndimbo alisema baada ya kuona kuna matumizi mengine ya uwanja na mudu ule ule wa mechi waliamua kubadilisha na kuupeleka Uwanja wa Uhuru kwani ulikuwa hauna matumizi yoyote kwa muda huo wa saa 10:00 jioni "Ni mabadiliko ya kawaida tu pale inapotokea, mabadiliko kama haya yanakuwa nje ya uwezo wetu kwa maana hiyo mechi itachezwa saa 10:00 jioni uwanja wa Uhuru na si Taifa kama ilivyokuwa hapo awali," alisema "Ratiba za mechi nyingine zitabaki vile vile kama ambavyo tulipanga hapo awali na mabadiliko yamefanyika mchezo wa Simba kutokana na sababu hiyo ambayo tumeeleza," alisema Ndimbo.

Chanzo: mwananchi.co.tz