Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Nkana na UD Songo ndio itakayoamua nani acheze na Simba

30165 Pic+simba TanzaniaWeb

Wed, 5 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

MECHI ya kesho kati ya Nkana Red Devils ya Zambia na UD Songo ya Msumbiji ndio itakayoamua nani acheze na Simba hatua ya pili katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba imeingia hatua ya pili baada ya kuwafunga Mbabane Swallows mabao 4-1 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam pia wakiibuka na ushindi wa mabao 4-0 ugenini. Mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama (mawili),Meddie Kagere, na Emmanuel Okwi. Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Hassan Kessy anaichezea timu ya Nkana Red Devils na kama itashinda mechi dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, itakuwa rahisi kwa Wanamsimbazi kujua siri ya wapinzani wao. Kessy amewahi kukaririwa na Mwanaspoti akisema klabu yake ya Nkana Red Devils wanajua kujituma uwanjani inayotokana na wachezaji kulinda nafasi zao za kucheza. "Soka ni lile lile, ila huku mchezaji anayecheza kikosi cha kwanza anajua kulinda heshima yake, ndio maana hata mimi niliingia moja kwa moja kwenye mpango wa kocha, soka wanalichukulia kama kazi kweli kweli,"anasema.  

Chanzo: mwananchi.co.tz