Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kigoma Malima amesema amefanya jitihada za hali na mali kuhakikisha mechi ya Mtimbwa Sugar na Simba SC inapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro badala ya Manungu.
Malima amesema lengo la kufanya hivyo ni kifanya Mtibwa Sugar kuwa timu ya nyumbani hivyo popote itakapochezwa katika mkoa huo, mashabiki wajisikie ni timu ya nyumbani.
"Tunafanya hivi ili kuonesha umoja. Tunataka kila mwana Morogoro aione Mtibwa ni timu ya nyumbani hivyo tumeshafanya mazungumzo na wahusika ili mechi hii ya kwanza ipigwe hapa Jamhuri Morogoro," alisema Malima.
Mtibwa na Simba wanatarajia kucheza mechi yao ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2023-24 Agosti 17, mwaka huu.
MALIMA ATOA NENO KUHUSU MTIBWA: “Tuifanye Mtibwa iwe timu ya nyumbani’ maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kigoma Malima akizungumzia mipango yake ya kuhakikisha Uwanja wa Jamhuri Morogoro unatumika kwa mechi za NBC Premier League ambayo inaanza leo kutimua vumbi.
— Azam TV (@azamtvtz) August 15, 2023
Mkuu huyo… pic.twitter.com/0L5L7SYVLo