Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Ihefu Vs Yanga ilikuwa na ushamba mwingi - Jemedari

SAID JEMEDARI 1140x640 Mechi ya Ihefu Vs Yanga ilikuwa na ushamba mwingi - Jemedari

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Jemedari Said amezungumzia kitendo cha vijana waliokuwa wanabeba wachezaji waliopata majeraha kwenye mchezo wa Ihefu F dhidi ya Yanga SC hawakufanya kazi yao kwa usahihi.

Amesema suala hilo limeharibu kabisa ubora wa mchezo na kuitia dosari Ligi Kuu ya NBC ambayo ni ya tano kwa ubora Afrika.

"Identity ya Ligi yetu na soka la Tanzania ni muhimu sana, tunapaswa kuonyesha weledi kwenye mambo mengi ikiwa timefungwa, tumeshinda au vinginevyo.

"Angalia wale watoa huduma ya kwanza walivyobeba mgonjwa na mwendo wao, wanavyochelewa kuingia kiwanjani kuhudumia mgonjwa mpaka wachezaji wa timu pinzani wanataka kumtoa mgonjwa.

"Mechi imekosa hali ya uanamichezo na kuichafua hata slogan ya PLAY FAIR, BE POSITIVE.

"Kuwa fair ukiwa unaongoza au umefungwa, kuwa positive wakati wote ndo soka hasa kwenye Ligi namba 5 kwa ubora Afrika.

Kwenye mechi kulikuwa na ushamba mwingi sana ambao kuuona kwenye TV inachukiza."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live