Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi tatu za raundi ya tatu kusimama dakika moja kuombeleza

Almasi Kasongooo Mechi tatu za raundi ya tatu kusimama dakika moja kuombeleza

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania 'TPLB'imetoa maagizo kwa wasimamizi wa michezo iliyosalia ya raundi ya tatu baada ya kutokea kwa ajali ya basi lilikuwa na mashabiki wa Namungo Fc na kusababisha vifo na majeruhi.

Bodi ya Ligi imewaagiza wasimamizi hao kutumia muda wa moja kabla ya mchezo kuanza kama ishara ya kuomboleza Vifo vya mashabiki wanne waliofariki katika ajali hiyo.

"Kufuatia ajali hiyo Bodi inawaelekeza wasimamizi wa michezo yote mitatu iliyosalia kwenye mzunguko wa tatu kuhakikisha timu zinasimama dakika moja kabla ya mchezo kuanza kama ishara ya kuomboleza Vifo vya mashabiki hao".

Aidha Bodi inatoka pole kwa uongozi wa Namungo, mashabiki, familia na wote walioguswa na msiba huo na kuwatakia nafuu ya mapema majeruhi wote.

Mashabiki hao walikuwa wakisafiri kwenda Dar es salaam kwenye mchezo utakao wahusisha Namungo Fc akiwa ugenini dhidi ya Yanga katika uwanja wa Azam Complex Leo saa moja usiku.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: