Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi tano za Ligi Kuu zampa mzuka Manyasi, ajipanga tena

Manyasi Mechi tano za Ligi Kuu zampa mzuka Manyasi, ajipanga tena

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kucheza mechi tano za Ligi Kuu msimu huu, kiungo wa Ihefu, Geofrey Manyasi amesema malengo yake msimu huu ni kuwa katika kiwango bora ambacho kitamfanya aweze kucheza michezo yote 30 ya mashindano hayo.

Kiungo huyo amesajiliwa msimu huu na Ihefu akitokea Geita Gold ambapo mpaka sasa ameshacheza michezo mitano ya Ligi Kuu na kuwa mmoja ya wachezaji ambao wameaminiwa na benchi la ufundi la timu hiyo.

Manyasi amesema anashukuru ameanza vizuri na lengo lake ni kuendelea kujituma zaidi ili aendelee kuaminiwa na benchi la ufundi kwenye kikosi cha kwanza.

Amesema mkakati wake msimu huu ni kuhakikisha anacheza mechi zote za Ligi Kuu ambapo anaamini kujituma kwake na kuwa katika kiwango bora kitafanya malengo hayo yaweze kutimia akiwa na kikosi hicho.

“Ni jambo nzuri kwangu nimeanza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza baada ya kutua hapa ni kitu kizuri kwangu nimecheza mechi tano za Ligi Kuu hivyo kwangu natamani zaidi nicheze mechi zote msimu huu,” alisema Manyasi na kuongeza;

“Kikubwa ninachokifanya sasa ni kufanya mazoezi ya nguvu ambayo yatanifanya niwe fiti kwa kila mchezo nitakaocheza wa ligi kitu ambacho kitafanya kocha aendelee kuniamini na kunipanga maana kwenye kikosi chetu tupo zaidi ya viungo wanne hivyo ni lazima nikaze sana.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: